Al-Ahzaab 33:55
الأحزابلَّا جُنَاحَ عَلَيْهِنَّ فِىٓ ءَابَآئِهِنَّ وَلَآ أَبْنَآئِهِنَّ وَلَآ إِخْوَٰنِهِنَّ وَلَآ أَبْنَآءِ إِخْوَٰنِهِنَّ وَلَآ أَبْنَآءِ أَخَوَٰتِهِنَّ وَلَا نِسَآئِهِنَّ وَلَا مَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُهُنَّ ۗ وَٱتَّقِينَ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدًا
Hapana ubaya kwao (wake za Mtume), kuonana na baba zao, wala watoto wao, wala kaka zao, wala watoto wa kiume wa kaka zao, wala watoto wa kiume wa dada zao, wala wanawake wenzao, wala wale waliomilikiwa na mikono yao ya kulia. Na enyi wanawake, mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hapana ubaya kwao (wake za Mtume) kuonana na baba zao, wala watoto wao, wala ndugu zao, wala watoto wa ndugu zao wanaume, wala watoto wa ndugu zao wanawake, wala wanawake wenzao, wala wale iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Na enyi wanawake, mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu. [55]
[55] Hapana dhambi kwa wakeze Nabii wakitojificha kwa baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au watoto wa ndugu zao wa kiume, au watoto wa ndugu zao wa kike, au wanawake Waumini wenginewe, au watumwa walio wamiliki, kwa sababu ya shida ya kuwahitajia kwa matumishi. Nanyi wanawake, mcheni Mwenyezi Mungu katika mambo aliyo kuamrisheni, wala msipindukie mipaka yake. Kwani Yeye hakika anajua kila kitu, hapana kilicho fichikana kwake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuna dhambi kwa wanawake kutojifunika mbele ya baba zao, watoto wao wa kiume,ndugu zao wa kiume, watoto wa kiume wa ndugu zao wa kiume, watoto wa kiume wa ndugu zao wa kike, wanawake waumini na watumwa waliomilikiwa na wao kwa kuwa wanahitaji utumishi wao sana. Na muogopeni Allah Mtukufu, enyi wanawake, msipite mpaka mliowekewa mkaonyesha pambo lenu lisilofaa kulionyesha, au mkaacha kujifunika mbele ya yule ambaye ni lazima mjifunike mbele yake. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kushuhudia kila kitu, Anashuhudia matendo ya waja, ya nje na ya ndani, na Atawalipa kwayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net