Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 54

Al-Ahzaab 33:54

الأحزاب

إِن تُبْدُوا۟ شَيْـًٔا أَوْ تُخْفُوهُ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمًا

Maana

Mkidhihirisha chochote kile, au mkikificha, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mkidhihirisha chochote kile, au mkikificha, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu. [54]

[54] Mkidhihirisha walau kidogo katika mambo yanayo muudhi, au mkikificha katika vifua vyenu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mkidhihirisha chochote kwa ndimi zenu, enyi watu, kati ya vitu vinavyomkera Mtume katika vile alivyowakataza navyo au mkakificha ndani ya nafsi zenu, basi Allah Mtukufu, aliyetukuka anavijua vilivyomo ndani ya nyoyo zenu na vile mlivyovidhihirisha, na Atawalipa kwa hayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net