Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 19

Al-Ahzaab 33:19

الأحزاب

أَشِحَّةً عَلَيْكُمْ ۖ فَإِذَا جَآءَ ٱلْخَوْفُ رَأَيْتَهُمْ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ تَدُورُ أَعْيُنُهُمْ كَٱلَّذِى يُغْشَىٰ عَلَيْهِ مِنَ ٱلْمَوْتِ ۖ فَإِذَا ذَهَبَ ٱلْخَوْفُ سَلَقُوكُم بِأَلْسِنَةٍ حِدَادٍ أَشِحَّةً عَلَى ٱلْخَيْرِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَمْ يُؤْمِنُوا۟ فَأَحْبَطَ ٱللَّهُ أَعْمَـٰلَهُمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرًا

Maana

Wana choyo juu yenu. Ikifika hofu, utawaona wanakutazama na macho yao yanazunguka, kama yule ambaye alizimia kwa kukaribia mauti. Na hofu ikiondoka, wanawaudhi kwa ndimi kali, nao ni mabahili kwa kila la heri. Hao hawakuamini, basi Mwenyezi Mungu amevibatilisha vitendo vyao. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wana choyo juu yenu. Ikifika khofu utawaona wanakutazama na macho yao yanazunguka, kama yule ambaye aliye zimia kwa kukaribia mauti. Na khofu ikiondoka wanakuudhini kwa ndimi kali, nao ni mabakhili kwa kila la kheri. Hao hawakuamini, basi Mwenyezi Mungu amevibat'ilisha vitendo vyao. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. [19]

[19] Wana pupa juu yenu kwa kuonekana dhaahiri inapo kuwa hapana khofu. Na ikija khofu ya adui au ya Mtume s.a.w. utawaona wanakuangalia na macho yao yanawazunguka hawajitambui, kama hali ya mwenye kuzimia wakati wa sumbuko la kukaribia mauti. Na khofu ikiondoka wanapita mpaka kukutukaneni na kukushutumuni kwa ndimi za kukata. Hao ni mabakhili kwa kila la kheri. Hao hawakuamini kwa nyoyo zao, ijapo kuwa wametangaza kuwa ni Waislamu. Basi Mwenyezi Mungu amezibat'ilisha a'mali zao kwa ukafiri wao walio dhamiria. Na kubat'ilisha huko ni jambo jepesi kwa Mwenyezi Mungu. Aya hii tukufu inaashiria ukweli wa kisayansi ambao ulikuwa haukujuulikana namna yake wakati wa kuteremka Qur'ani Tukufu. Ukweli huo ni kuwa jicho wakati wa kukurubia mauti au wakati wa khofu huzunguka. Na katika sababu za hayo ni kuwa kwa shida ya khofu utambuzi hutoweka, ikawa mtu hajitambui. Vituo vya navo zisio tambua katika ubongo hupoteza mizani yake, basi huwa huyo mwenye khofu kama mfano wa mwenye kuzimia kwa kukaribia kufa, jicho lake huzunguka na mboni ya jicho hupanuka, na hubaki katika hali ya kukodoa macho mpaka kufa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wanawafanyia nyinyi, enyi Waumini, ugumu wa mali, nafsi, juhudi na mapenzi kwa uadui na chuki walizonazo ndani ya nafsi zao, kwa kupenda kuishi na kuogopa kufa. Na vita vikisimama huwa wakiogopa kuangamia, na utawaona wanakuangalia, macho yao yanazunguka kwa kuwa akili zao zimeondoka kwa kuogopa na kukimbia kuuawa, kama vile macho ya mtu aliyekaribia kufa yanavyozunguka. Na vita vinapomalizika na hofu kuondoka wanawarushia nyinyi matamshi makali yenye kukera. Na utawakuta wao, zinapogawiwa ngawira, ni wachoyo na ni mahasidi. Hao hawakuamini kwa nyoyo zao ndipo Allah Mtukufu Akawaondolea thawabu za matendo yao, na hilo kwa Allah Mtukufu ni jepesi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net