Al-Ahzaab 33:20
الأحزابيَحْسَبُونَ ٱلْأَحْزَابَ لَمْ يَذْهَبُوا۟ ۖ وَإِن يَأْتِ ٱلْأَحْزَابُ يَوَدُّوا۟ لَوْ أَنَّهُم بَادُونَ فِى ٱلْأَعْرَابِ يَسْـَٔلُونَ عَنْ أَنۢبَآئِكُمْ ۖ وَلَوْ كَانُوا۟ فِيكُم مَّا قَـٰتَلُوٓا۟ إِلَّا قَلِيلًا
Wanafikiri yale makundi ya maadui hayajaondoka. Na yakija hayo makundi, watatamani laiti wao wako majangwani pamoja na mabedui, wakiuliza habari zenu. Na lau wangekuwa pamoja nanyi, basi hawangepigana isipokuwa kidogo tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanafikiri yale makundi ya maadui hayajaondoka. Na yakija hayo makundi watatamani laiti wao wako majangwani pamoja na mabedui, wakiuliza khabari zenu. Na lau wakiwa pamoja nanyi hawapigani ila kidogo tu. [20]
[20] Wanadhani hawa wanaafiki kwamba majeshi ya makafiri yaliyo ungana bado yapo mahali pao wanaizinga Madina. Na hayo makundi ya maadui yakirejea tena, watatamani hao woga laiti wangeli kuwa wanaishi pamoja na mabedui huko majangwani wakidondoa khabari zenu. Na lau wakibaki kwenye kambi zao, na wasikimbie, na majeshi mawili yakapambana, basi hata hivyo wasinge pigana pamoja nanyi ila kidogo tu, kama kujionyesha na watajwe kuwa nao walikuwamo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanafiki wanadhani kwamba makundi ya watu ambao Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Aliwafanya washindwe, hawakuondoka kwenda zao, hivyo ni kwa sababu ya uoga. Na lau hayo mapote yangerudi Madina wangetamani wanafiki hao kuwa wao hawako Madina, wako pamoja na mabedui wa jangwani wanatafuta habari zenu wakiwa mbali. Na lau wangekua wako na nyinyi wasingepigana pamoja na nyinyi isipokuwa kidogo, kwa uoga wao mwingi, unyonge wao na uchache wa Imani yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net