Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 21

Al-Ahzaab 33:21

الأحزاب

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِى رَسُولِ ٱللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُوا۟ ٱللَّهَ وَٱلْيَوْمَ ٱلْـَٔاخِرَ وَذَكَرَ ٱللَّهَ كَثِيرًا

Maana

Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anayemtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana. [21]

[21] Hakika nyinyi mna kiigizo kizuri kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa mwenye kutaraji rehema ya Mwenyezi Mungu, na neema za Siku ya Mwisho, na akamkumbuka na kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika khofu na kutumai, na katika shida, na katika neema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika yenu nyinyi, enyi Waumini, mna mfano mwema wa kuiga katika maneno ya Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), matendo yake na mwenendo wake. Basi jilazimisheni na mwenendo wake, kwani anayeufuata na kuuiga ni yule anayemtaraji Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho, Akamtaja Allah Mtukufu na kumuomba msamaha kwa wingi na akamshukuru kwa kila namna.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net