Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 22

Al-Ahzaab 33:22

الأحزاب

وَلَمَّا رَءَا ٱلْمُؤْمِنُونَ ٱلْأَحْزَابَ قَالُوا۟ هَـٰذَا مَا وَعَدَنَا ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَصَدَقَ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ ۚ وَمَا زَادَهُمْ إِلَّآ إِيمَـٰنًا وَتَسْلِيمًا

Maana

Na Waumini walipoyaona makundi, walisema, "Haya ndiyo aliyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli." Na hayo hayakuwazidisha ila Imani na utiifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Waumini walipo yaona makundi, walisema: Haya ndiyo aliyo tuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli. Na hayo hayakuwazidisha ila Imani na ut'iifu. [22]

[22] Na Waumini walipo yaona makundi ya washirikina walisema: Haya ndiyo aliyo tuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake zamani. Kwani walituahidi tutapata shida, na kisha tutapata ushindi. Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli. Taabu hizi basi, hazikuwazidishia ila nguvu za kumuamini Mwenyezi Mungu, na uzuri wa kuinyenyekea kwao hukumu yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Waumini walipoyashuhudia mapote ya watu waliojikusanya pembeni mwa mji wa Madina na wakauzunguka, walikumbuka kwamba ahadi ya ushindi imekaribia na wakasema, «Haya ndiyo yale Aliyotuahidi Allah Mtukufu na Mtume Wake ya maonjo, shida na (kisha) ushindi. Allah Mtukufu Alitekeleza ahadi Yake na Mtume Wake alisema kweli katika bishara njema aliyoitoa. Na hakukuwaongezea kule kuyatazama yale mapote isipokuwa kumuamini Allah Mtukufu na kujisalimisha na uamuzi Wake na kufuata amri Yake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net