Al-Ahzaab 33:18
الأحزابقَدْ يَعْلَمُ ٱللَّهُ ٱلْمُعَوِّقِينَ مِنكُمْ وَٱلْقَآئِلِينَ لِإِخْوَٰنِهِمْ هَلُمَّ إِلَيْنَا ۖ وَلَا يَأْتُونَ ٱلْبَأْسَ إِلَّا قَلِيلًا
Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawajua hao wanaozuilia, na wanaowaambia ndugu zao: "Njooni kwetu!" Wala hawaingii vitani isipokuwa kidogo tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawajua hao wanao zuilia, na wanao waambia ndugu zao: Njooni kwetu! Wala hawaingii vitani ila kidogo tu. [18]
[18] Hakika Mwenyezi Mungu anawajua wanao zuilia miongoni mwenu, na wanao waambia ndugu zao: Unganeni nasi! Wala hawaingii katika vita vinapo shitadi ila kidogo tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Allah Mtukufu Anawajua wale wenye kuwavunja watu moyo wasipigane jihadi katika njia ya Allah Mtukufu, na wenye kuwaambia ndugu zao, «Njooni mjiunge na sisi na muacheni Muhammad! Msihudhurie vitani pamoja naye.» Kwani sisi tunachelea msije mkaangamia anapoangamia yeye. Na wao, pamoja na uvunjaji moyo wao huu, hawaji vitani isipokuwa kwa karaha, kwa kujionyesha na kutaka kusikika na kuogopa fedheha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net