Al-Ahzaab 33:17
الأحزابقُلْ مَن ذَا ٱلَّذِى يَعْصِمُكُم مِّنَ ٱللَّهِ إِنْ أَرَادَ بِكُمْ سُوٓءًا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ رَحْمَةً ۚ وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا
Sema: Ni nani wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu pindi akiwatakia uovu, au akiwatakia rehema? Wala hawatapata mlinzi wala msaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Ni nani wa kukulindeni na Mwenyezi Mungu pindi akikutakieni uovu, au akikutakieni rehema? Wala hawatapata mlinzi wala msaidizi isipo kuwa Mwenyezi Mungu. [17]
[17] Waambie hawa wanao babaika: Nani atakaye kulindeni na Mwenyezi Mungu akitaka kukuleteeni shari, au atakaye kuzuieni msipate kheri, akitaka Yeye kukurehemuni? Wala hawatapata badala ya Mwenyezi Mungu yeyote wa kuwalinda au kuwaokoa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Nabii, kuwaambia, «Ni nani Atakayewazuia na Allah Mtukufu Au Atakayewaokoa na adhabu Yake Akiwa Anawatakia ubaya au Akiwa Anawatakia rehema?» Na hakika Yeye Ndiye Mpaji, Mzuiliaji, Mwenye kudhuru, Mwenye kunufaisha? Na hawatapata hawa wanafiki, isipokuwa Allah Mtukufu, msaidizi wa kuwasaidia wala mnusuru wa kuwapa ushindi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net