Al-Ahzaab 33:16
الأحزابقُل لَّن يَنفَعَكُمُ ٱلْفِرَارُ إِن فَرَرْتُم مِّنَ ٱلْمَوْتِ أَوِ ٱلْقَتْلِ وَإِذًا لَّا تُمَتَّعُونَ إِلَّا قَلِيلًا
Sema: Kukimbia hakuwafai kitu ikiwa mnakimbia mauti au kuuawa, na hata hivyo hamtastareheshwa isipokuwa kidogo tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Kukimbia hakukufaeni kitu ikiwa mnakimbia mauti au kuuwawa, na hata hivyo hamtastareheshwa ila kidogo tu. [16]
[16] Waambie: Kukimbia hakukufaeni kitu ikiwa ndio mnayakimbia mauti au kuuwawa, maadamu ajali yenu imekwisha fika. Na ikiwa haijafika, basi hamtobaki mkistarehe katika dunia ila kwa muda wa umri wenu, nao ni mchache.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Nabii, kuwaambia hawa wanafiki, «Kukimbia kwenu vitani kwa kuogopa kufa au kuuawa, huko hakutachelewesha muda wenu wa kuishi katika dunia hii, na mkikimbia hamtastarehe katika dunia hii isipokuwa kwa kadiri ya umri wenu uliowekewa kikomo, nacho ni muda mchache sana ukilinganishwa na Akhera».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net