Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 15

Al-Ahzaab 33:15

الأحزاب

وَلَقَدْ كَانُوا۟ عَـٰهَدُوا۟ ٱللَّهَ مِن قَبْلُ لَا يُوَلُّونَ ٱلْأَدْبَـٰرَ ۚ وَكَانَ عَهْدُ ٱللَّهِ مَسْـُٔولًا

Maana

Na hakika walikwisha muahidi Mwenyezi Mungu kabla yake kwamba hawatageuza migongo yao. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika walikwisha muahidi Mwenyezi Mungu kabla yake kwamba hawatageuza migongo yao. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa. [15]

[15] Na hakika hawa wenye kukimbia kutoka midani ya vita walikwisha muahidi Mwenyezi Mungu kabla yake kuwa watasimama imara katika vita pamoja na Mtume, na wala hawatakimbia. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa kwa yule mwenye kuitoa, na yampasa aitimize.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa hakika, wanafiki hawa walimuahidi Allah Mtukufu kupitia kwa Mtume Wake kabla ya vita vya Shimo (Khandaq ) kuwa hawatakimbia watakapohudhuria vita na hawatachelewa watakapoitwa kwenda Jihadi, lakini wao walihini ahadi yao. Na Allah Mtukufu Atawahesabu kwa hilo na Atawauliza kuhusu ahadi hiyo. Hakika ahadi ya Allah Mtukufu itaulizwa na itahesabiwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net