Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 14

Al-Ahzaab 33:14

الأحزاب

وَلَوْ دُخِلَتْ عَلَيْهِم مِّنْ أَقْطَارِهَا ثُمَّ سُئِلُوا۟ ٱلْفِتْنَةَ لَـَٔاتَوْهَا وَمَا تَلَبَّثُوا۟ بِهَآ إِلَّا يَسِيرًا

Maana

Na lau kuwa wangeliingiliwa kwa pande zote, kisha wakatakiwa kufanya hiana, wangelifanya, na wasingelisita isipokuwa kidogo tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau kuwa wangeli ingiliwa kwa pande zote, kisha wakatakiwa kufanya khiana, wangeli fanya, na wasingeli sita ila kidogo tu. [14]

[14] Lau kuwa makundi ya majeshi ya maadui wangeli waingilia Madina kwa kila upande, na wakawataka watangaze kuwa wameuwacha Uislamu na wawapige vita Waislamu bila ya shaka wangeli wakubalia yale waliyo takiwa, na wala wasingeli sita ila muda mfupi tu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau jeshi la makundi lingeingia Madina kupitia pembezoni mwake, kisha wakatakwa hawa wanafiki wamshirikishe Allah Mtukufu na warudi kutoka kwenye Uislamu, wangekubali hilo kwa haraka, na wasingechelewesha kurudi kwenye ushirikina isipokuwa kwa muda mchache.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net