Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 13

Al-Ahzaab 33:13

الأحزاب

وَإِذْ قَالَت طَّآئِفَةٌ مِّنْهُمْ يَـٰٓأَهْلَ يَثْرِبَ لَا مُقَامَ لَكُمْ فَٱرْجِعُوا۟ ۚ وَيَسْتَـْٔذِنُ فَرِيقٌ مِّنْهُمُ ٱلنَّبِىَّ يَقُولُونَ إِنَّ بُيُوتَنَا عَوْرَةٌ وَمَا هِىَ بِعَوْرَةٍ ۖ إِن يُرِيدُونَ إِلَّا فِرَارًا

Maana

Na kundi moja katika miongoni mwao liliposema: "Enyi watu wa Yathrib, hapana kukaa nyinyi! Rudini." Na kundi jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Nabii kwa kusema: "Hakika nyumba zetu ni tupu." Wala hazikuwa tupu; hawakutaka isipokuwa kukimbia tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kundi moja katika miongoni mwao lilipo sema: Enyi watu wa Yathrib! Hapana kukaa nyinyi! Rudini. Na kundi jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Mtume kwa kusema: Hakika nyumba zetu ni tupu. Wala hazikuwa tupu; hawakutaka ila kukimbia tu. [13]

[13] Na kumbuka walipo sema kikundi cha wanaafiki na ambao wanao rega rega: Enyi watu wa (Yathrib, yaani) Madina! Hapana maana kubakia hapa nyinyi katika vita hivi vya kushindwa. Rudini mwende makwenu. Na kundi jingine kati yao walimtaka ruhusa Mtume warejee Madina, na wakasema: Hakika nyumba zetu hazina ulinzi. Hatuna budi kurejea tukazilinde. Wala nyumba zao hazikuwa khatarini kabisa kama walivyo sema. Hawakutaka ila kukimbia vita tu, kwa udhuru wa uwongo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Nabii, neno la kikundi cha wanafiki wakiwaita Waumini miongoni mwa watu wa Madina, «Enyi watu wa Yathrib (nalo ni jina la zamani la Madina), ‘Msikae kwenye vita ambavyo mtashindwa, rudini majumbani mwenu ndani ya Madina’» Na pote lingine la wanafiki linamuomba ruhusa Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kurudi majumbani mwao kwa kisingizio kuwa hayako imara, na kwa hivyo wanayaogopea, na ukweli ni kwamba hayo si hivyo, na lengo lao halikuwa isipokuwa ni kukimbia vita.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net