Al-Ahzaab 33:12
الأحزابوَإِذْ يَقُولُ ٱلْمُنَـٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ مَّا وَعَدَنَا ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥٓ إِلَّا غُرُورًا
Na waliposema wanafiki na wale wenye maradhi katika nyoyo zao: "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walipo sema wanaafiki na wale wenye maradhi katika nyoyo zao: Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu. [12]
[12] Na kumbuka shaka iliyo waingia wanaafiki na wagonjwa wa nyoyo walipo sema: Ahadi aliyo tupa Mwenyezi Mungu na Mtume ni ahadi ya uwongo, imekusudiwa kutudanganya tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na pindi waliposema wanafiki na wale ambao ndani ya nyoyo zao mna shaka, nao ni wale madhaifu wa Imani, «Ahadi ya Allah Mtukufu Aliyotuahidi ya kupata ushindi na utulivu, haikuwa isipokuwa ni maneno ya urongo na udanganyifu, basi msimuamini».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net