Al-Ahzaab 33:11
الأحزابهُنَالِكَ ٱبْتُلِىَ ٱلْمُؤْمِنُونَ وَزُلْزِلُوا۟ زِلْزَالًا شَدِيدًا
Hapo ndipo Waumini walipojaribiwa, na wakatikiswa mtikiso mkali.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hapo ndipo Waumini walipo jaribiwa, na wakatikiswa mtikiso mkali. [11]
[11] Katika wakati ule Waumini walifanyiwa mtihani juu ya kusubiri kwao juu ya Imani. Wakatikisika kwa khofu kwa mtikiso mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Katika msimamo huo mgumu, Imani za Waumini zilijaribiwa na watu wakakaguliwa, na akajulikana mnafiki kwa kutengwa na Muumini, na wakasukikasukika msukosuko mkali kwa kuingiwa na woga na babaiko, ili Imani yao ibainike na yakini yao izidi
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net