Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 10

Al-Ahzaab 33:10

الأحزاب

إِذْ جَآءُوكُم مِّن فَوْقِكُمْ وَمِنْ أَسْفَلَ مِنكُمْ وَإِذْ زَاغَتِ ٱلْأَبْصَـٰرُ وَبَلَغَتِ ٱلْقُلُوبُ ٱلْحَنَاجِرَ وَتَظُنُّونَ بِٱللَّهِ ٱلظُّنُونَا۠

Maana

Walipowakujieni kutoka juu yenu, na kutoka chini yenu; na macho yalipokodoka, na nyoyo zikapanda kooni, nanyi mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbalimbali.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walipo kujieni kutoka juu yenu, na kutoka chini yenu; na macho yalipo kodoka, na nyoyo zikapanda kooni, nanyi mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali. [10]

[10] Walipo kujieni kutoka upande wa juu ya bonde, na kutoka chini, na macho yakakodoka, na nyoyo zikapanda mpaka kwenye koo, kwa kufazaika na kubabaika. Na nyinyi katika wakati ule wa shida kubwa kila namna ya dhana zilikujieni juu ya ahadi ya Mwenyezi Mungu. Si makusudio ya maneno haya kuwa maadui walikuja kutoka kila upande. Tukiangalia ufafanuzi wa tukio hili inadhihirika kuwa makusudio ni kuwa walio kuja kutoka upande wa juu ya Waislamu, ni kabila ya Ghat'fan na walio wafuata katika wakaazi wa Najdi, kwani wao walikuja pande za juu ya Bara Arabu upande wa mashariki. Na inatudhihirikia kuwa walio kuja upande wa chini ya Waumini ni Makureshi, kwa sababu wao walikuja kutoka upande wa chini ya Bara Arabu upande wa magharibi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kumbukeni pindi walipowajia kwa juu yenu kutoka sehemu ya juu ya bonde lililoko upande wa mashariki na kwa chini yenu kutoka sehemu ya kati ya bonde lililoko upande wa magharibi, na pindi macho yalipokodoka kwa kuduwaa sana na kushtuka, na nyoyo zikafika kwenye makoromeo kwa kitisho kikali, na wanafiki wakajawa na ukataji tamaa na uvumi ukazidi, na mkawa mnamdhania Allah Mtukufu dhana mbaya ya kuwa Yeye Hataiokoa Dini Yake na Hatalikuza jina Lake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net