Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 9

Al-Ahzaab 33:9

الأحزاب

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱذْكُرُوا۟ نِعْمَةَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَآءَتْكُمْ جُنُودٌ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا وَجُنُودًا لَّمْ تَرَوْهَا ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا

Maana

Enyi mlioamini, zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu. Pale yalipokufikieni majeshi, nasi tukayapelekea upepo, na majeshi msiyoyaona. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilio juu yenu. Pale yalipo kufikilieni majeshi, nasi tukayapelekea upepo, na majeshi msiyo yaona. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda. [9]

[9] Enyi mlio amini zikumbukeni neema na fadhila za Mwenyezi Mungu zilio juu yenu, pale yalipo kujieni makundi katika Siku ya Handaki. Tukawapelekea upepo mkali wa kimbunga ubaridi, na Malaika ambao nyinyi hamwaoni. Kikawaingia kiwewe katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu alikuwa Mwenye kuviona vitendo vyenu, na ukweli wa niya zenu. Basi akaingia kukulindeni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi Waumini! Ikumbukeni neema ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Aliyowaneemesha nyinyi katika Madina siku ya vita vya Makundi (Aḥzāb), navyo ndivyo vita vya Shimo (Khandaq), walipojikusanya dhidi yenu washirikina kutoka nje ya Madina, na Mayahudi na wanafiki wakiwa ndani ya Madina na pembezoni mwake, wakawazunguka nyinyi, hapo tukayatumia yale makundi upepo mkali uliong’oa mahema yao na kuvirusha vyungu vyao, na tukawatumia Malaika kutoka mbinguni msiowaona, hapo basi nyoyo zao zikaingia woga. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuyaona mnayoyatenda, hakuna chochote kinachofichika kwake katika hayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net