Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 8

Al-Ahzaab 33:8

الأحزاب

لِّيَسْـَٔلَ ٱلصَّـٰدِقِينَ عَن صِدْقِهِمْ ۚ وَأَعَدَّ لِلْكَـٰفِرِينَ عَذَابًا أَلِيمًا

Maana

Ili Mwenyezi Mungu awaulize wakweli juu ya ukweli wao. Na amewaandalia makafiri adhabu chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ili (Mwenyezi Mungu) awaulize wakweli juu ya ukweli wao. Na amewaandalia makafiri adhabu chungu. [8]

[8] Ili Mwenyezi Mungu awaulize Manabii Siku ya Kiyama juu ya waliyo waambia kaumu zao. Na Yeye amewaandalia wenye kuwakataa Mitume adhabu yenye kutia uchungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Alichukua ahadi hiyo kutoka kwa Mitume hao, ili Apate kuwauliza waliotumwa vile walivyojibiwa na ummah wao, ili Allah Mtukufu Awalipe Pepo wenye kuamini. Na Amewaandalia makafiri, Siku ya Kiyama, adhabu kali ndani ya Jahanamu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net