Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 7

Al-Ahzaab 33:7

الأحزاب

وَإِذْ أَخَذْنَا مِنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ مِيثَـٰقَهُمْ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٍ وَإِبْرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَى ٱبْنِ مَرْيَمَ ۖ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَـٰقًا غَلِيظًا

Maana

Na tulipochukua ahadi kwa Manabii na kwako wewe, na Nuhu na Ibrahim na Isa mwana wa Mariamu, na tulichukua kwao ahadi ngumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tulipo chukua ahadi kwa Manabii na kwako wewe, na Nuhu na Ibrahim na Isa mwana wa Mariamu, na tulichukua kwao ahadi ngumu! [7]

[7] Na kumbusha pale tulipo fanya agano na Manabii wote walio tangulia kuwa watafikisha ujumbe na wito kulingania Dini iliyo sawa, na wewe, na Nuhu, na Ibrahim, na Musa, na Isa bin Maryamu; na tukachukua kwao agano lenye shani kubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Nabii, tulipochukua kutoka kwa Manabii ahadi ya mkazo kutekeleza ujumbe, na tukachukua ahadi kutoka kwako, na kutoka kwa Nūḥ, Ibrãhîm, Mûsã na Ῐsā mwana wa Maryam (nao ndio Mitume wenye nyoyo thabiti, katika kauli iliyo mashuhuri), na tukachukua kutoka kwao ahadi ya mkazo ya kufikisha ujumbe na kutekeleza amana na kuaminiana wao kwa wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net