Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 6

Al-Ahzaab 33:6

الأحزاب

ٱلنَّبِىُّ أَوْلَىٰ بِٱلْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ ۖ وَأَزْوَٰجُهُۥٓ أُمَّهَـٰتُهُمْ ۗ وَأُو۟لُوا۟ ٱلْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِى كِتَـٰبِ ٱللَّهِ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُهَـٰجِرِينَ إِلَّآ أَن تَفْعَلُوٓا۟ إِلَىٰٓ أَوْلِيَآئِكُم مَّعْرُوفًا ۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِى ٱلْكِتَـٰبِ مَسْطُورًا

Maana

Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao. Na jamaa ni karibu wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuliko Waumini wengine na Wahamiaji. Ila muwe mnawafanyia wema marafiki zenu. Haya yamekwisha andikwa Kitabuni.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao. Na jamaa ni karibu wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuliko Waumini wengine na Wahamiaji. Ila muwe mnawafanyia wema marafiki zenu. Haya yamekwisha andikwa Kitabuni. [6]

[6] Nabii Muhammad ni mwenye kustahiki zaidi urafiki kwa Waumini, na ana huruma zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Basi yawapasa wao wampende na wamt'ii. Na wake zake ni Mama zao kwa kuwatukuza na kuwahishimu, na kuwa ni haramu juu yao kuwaoa baada yake. Na jamaa walio khusiana ni karibu zaidi kuliko Waumini wenginewe na Wahajiri, walio hama Makka, kwa kurithiana wao kwa wao kama ilivyo wajibika katika Qur'ani. Lakini inafaa kumfanyia wema mlio fanya urafiki naye katika Dini asiye kuwa jamaa yenu, kwa kuwapa wema na mapenzi au hata kumuandikia mali katika wasia. Hayo ya kurithiana jamaa walio khusiana yamethibiti katika Kitabu cha Qur'ani wala hayawezi kubadilishwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nabii Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ni bora kwa Waumini na ni karibu na wao zaidi kuliko nafsi zao katika mambo ya dini na dunia. Na heshima ya wake wa Nabii, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa ummah wake, kama vile heshima ya mama zao, haifai kuwaoa wake za Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), baada yake. Na wenye ujamaa wa ukaribu, miongoni mwa Waislamu, baadhi yao wana haki zaidi ya kuwarithi wengine katika hukumu ya Allah Mtukufu na sheria Yake kuliko kurithi kwa (misingi ya) Imani na kuhama. (Waislamu hapo mwanzo wa Uislamu walikuwa wakirithiana kwa misingi ya hijrah (kuhama) na Imani au Dini na si kwa kizazi, kisha hilo likaondolewa kwa aya ya urithi), isipokuwa iwapo nyinyi, enyi Waislamu, mtawafanyia wema kwa kuwahami, kuwafanyia wema, kuwaunga na kuwaachia wasia wa kuwafaidisha. Hukumu hii iliyotajwa imekadiriwa, imeandikwa kwenye Ubao uliyohifadhiwa, basi ni lazima kwenu muifuate kivitendo. Ndani ya aya hii pana ulazima wa kuwa Mtume, (rehema na amani zimshukie), awe ni mwenye kupendwa zaidi na mja kuliko nafsi yake, na ulazima wa kumfuata yeye kikamilifu. Na ndani yake pana ulazima wa kuwaheshimu mama wa Waumini, wake wa Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na kwamba mwenye kuwatukana atarudi na hasara.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net