As-Sajda 32:25
السجدةإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ فِيمَا كَانُوا۟ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ
Hakika Mola wako Mlezi ndiye atakayefafanua baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana ndani yake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Mola wako Mlezi ndiye atakaye fafanua baina yao Siku ya Kiyama katika waliyo kuwa wakikhitalifiana. [25]
[25] Hakika Mola wako Mlezi ndiye peke yake atakaye hukumu baina ya Manabii na kaumu zao Siku ya Kiyama katika mambo wanayo khitalifiana.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Mola wako, ewe Mtume, Atatoa uamuzi baina ya Waumini na makafiri miongoni mwa Wana wa Isrãîl na wasiokuwa wao Siku ya Kiyama kwa uadilifu katika yale waliotafautiana juu yake miongoni mwa mambo ya dini, na Atamlipa kila binadamu kwa matendo yake kwa kuwatia watu wa Peponi Peponi na watu wa Motoni Motoni.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net