Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 24

As-Sajda 32:24

السجدة

وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا۟ ۖ وَكَانُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا يُوقِنُونَ

Maana

Na tukawafanya miongoni mwa waongozi wanaoongoa watu kwa amri yetu, waliposubiri na wakawa na yakini na Ishara zetu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukawafanya miongoni mwao waongozi wanao ongoa watu kwa amri yetu, walipo subiri na wakawa na yakini na Ishara zetu. [24]

[24] Na kutokana na Wana wa Israili tumejaalia wawepo Maimamu, waongozi, wa Dini, wasimame kuwaongoa watu, kwa kuitikia amri yetu kwa vile walivyo vumilia kuyatenda yaliomo katika Taurati, na wakawa wanazisadiki Ishara zetu ukomo wa kusadiki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tuliwafanya, miongoni mwa Wana wa Isrãîl, ni waongozi na walinganizi kwenye wema, watu wanawafuata na wao wanawalingania kwenye kumpwekesha Allah Mtukufu na kumuabudu Peke Yake na kumtii. Na walipata daraja hii ya juu waliposubiri juu ya amri za Allah Mtukufu, kuyaacha makemeo Yake na kuwalingania na kuvumilia kero katika njia Yake, na walikuwa wanaziamini kikweli aya za Allah Mtukufu na hoja Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net