Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 23

As-Sajda 32:23

السجدة

وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ فَلَا تَكُن فِى مِرْيَةٍ مِّن لِّقَآئِهِۦ ۖ وَجَعَلْنَـٰهُ هُدًى لِّبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ

Maana

Hakika Sisi tulikwisha mpa Musa Kitabu. Basi usiwe na shaka kuwa kakipokea. Na tukakifanya kuwa ni uongofu kwa Wana wa Israili.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Sisi tulikwisha mpa Musa Kitabu. Basi usiwe na shaka kuwa kakipokea. Na tukakifanya kuwa ni uwongofu kwa Wana wa Israili. [23]

[23] Na Sisi tulikwisha mpa Musa Taurati. Basi usiwe na shaka na kupokea kwa Musa Kitabu hicho. Na tumekijaalia Kitabu alicho teremshiwa Musa kiwe ni uwongofu kwa Wana wa Israili.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tulimletea Mûsã Taurati kama tulivyokuletea wewe, ewe Mtume, Qur’ani. Basi usiwe na shaka ya kukutana na Mûsã usiku wa Isrā’ (safari ya kwenda Bayt al- Maqdis) na Mi’rāj (safari ya kwenda mbinguni), na tukaifanya Taurati ni uongofu kwa Wana wa Isrãîl, Unawalingania kwenye haki na kwenye njia iliyonyooka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net