As-Sajda 32:22
السجدةوَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِـَٔايَـٰتِ رَبِّهِۦ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَآ ۚ إِنَّا مِنَ ٱلْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ
Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayekumbushwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi, kisha akazikataa? Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye kumbushwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi, kisha akazikataa? Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu. [22]
[22] Na hapana mtu yeyote aliye zidi udhaalimu kuidhulumu Haki na kuidhulumu nafsi yake, kuliko mtu anaye kumbushwa kwa Ishara za Mwenyezi Mungu na hoja zilizo wazi, kisha akaacha kuziamini juu ya kuwa ni wazi dhaahiri. Hakika Sisi tutajilipizia juu ya kila mkosefu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuna hata mmoja aliye dhalimu zaidi wa nafsi yake kuliko yule aliyekumbushwa dalili za Allah Mtukufu kisha akazipa mgongo zote, asiwaidhike kwa mawaidha yake, bali akayafanyia kiburi. Hakika sisi ni wenye kuwatesa wale wahalifu waliozipa mgongo aya za Allah Mtukufu na hoja Zake na wasinufaike nazo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net