Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 21

As-Sajda 32:21

السجدة

وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنَ ٱلْعَذَابِ ٱلْأَدْنَىٰ دُونَ ٱلْعَذَابِ ٱلْأَكْبَرِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

Maana

Na hakika tutawaonjesha katika adhabu hafifu kabla ya adhabu kubwa, huenda labda watarejea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tutawaonjesha adhabu khafifu kabla ya adhabu kubwa, huenda labda watarejea. [21]

[21] Na tunaapa: Hapana shaka tutawaonjesha duniani adhabu duni kabla hawajaifikia hiyo adhabu kubwa kabisa, nayo ni kudumu milele katika Moto. Huenda pengine watakao adhibiwa kwa hiyo adhabu duni watatubia, waache ukafiri wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tutawaonjesha, tena tutawaonjesha, hawa waasi wenye kukanusha adhabu ndogo ya matatizo, shida na misiba ya duniani kabla ya adhabu kubwa zaidi Siku ya Kiyama, ambako wataadhibiwa ndani ya moto wa Jahanamu, huenda wao wakarejea na wakatubia dhambi zao kwa Mola wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net