As-Sajda 32:26
السجدةأَوَلَمْ يَهْدِ لَهُمْ كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّنَ ٱلْقُرُونِ يَمْشُونَ فِى مَسَـٰكِنِهِمْ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ ۖ أَفَلَا يَسْمَعُونَ
Ee! Haijawabainikia kwamba kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, nao wanapita katika maskani zao hizo? Hakika katika hayo zipo Ishara. Basi, je, hawasikii?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Haijawabainikia kwamba kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, nao wanapita katika maskani zao hizo? Hakika katika hayo zipo Ishara. Basi, je, hawasikii? [26]
[26] Je! Kwani Mwenyezi Mungu aliwaacha walio wakadhibisha Mitume wao, na hakuwabainishia kwamba Yeye aliwahilikisha wengi katika kaumu zilizo watangulia, na wao wanapita kwenye majumba yao, na wanatembea kwenye maskani zao? Hakika katika hayo pana mawaidha ya kuwaonyesha Haki. Wao wameingiwa na uziwi, hawasikii mawaidha haya.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani haikuwabainikia hawa wenye kumkanusha Mtume ni mara ngapi tuliwaangamiza ummah waliotangulia kabla yao na huku wanatembea kwenye makazi yao, wakawa wanayaona waziwazi, kama vile watu wa Hûd, Ṣãliḥ na Lûṭ? Hakika katika hayo kuna alama na mawaidha ya kutolea ushahidi ukweli wa Mitume waliowajia na urongo wa ushirikina walionao wale waliokanusha. Basi kwani hawasikii, hawa wenye kuwakanusha Mitume, mawaidha ya Allah Mtukufu na dalili Zake wakapata kunufaika nayo?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net