As-Sajda 32:27
السجدةأَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّا نَسُوقُ ٱلْمَآءَ إِلَى ٱلْأَرْضِ ٱلْجُرُزِ فَنُخْرِجُ بِهِۦ زَرْعًا تَأْكُلُ مِنْهُ أَنْعَـٰمُهُمْ وَأَنفُسُهُمْ ۖ أَفَلَا يُبْصِرُونَ
Je, hawaoni ya kwamba tunayapeleka maji kwenye ardhi kavu, kisha kwayo tunaitoa mimea wanayokula wanyama wao na wao wenyewe? Je, hawaoni?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Hawaoni ya kwamba tunayapeleka maji kwenye ardhi kavu, kisha kwayo tunaitoa mimea wanayo kula wanyama wao na wao wenyewe? Je! Hawaoni? [27]
[27] Wameingia upofu, na wala hawaoni ya kwamba hakika Sisi tunapeleka mvua na mito kwenye ardhi za ukame ambazo hazimei mimea, na tukaziotesha mazao yake, wakala wanyama wao, na wao wenyewe wakala nafaka zake na matunda yake? Wamepofuka, na kwa hivyo hawazioni dalili za Mwenyezi Mungu za kuwafufua wafu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani hawakuona wenye kukanusha kufufuliwa baada ya kufa kwamba sisi tunayapeleka maji kwenye ardhi kavu iliyo ngumu ambayo haina mimea, tukatoa kwa maji hayo mimea yenye rangi mbalimbali yenye kuliwa na wanyama wao na miili yao ikapata chakula cha kuwafanya wao waishi kwayo? Kwani hawazioni neema hizi kwa macho yao wakajua kwamba Allah Mtukufu ni Muweza wa kuwahuisha wafu na kuwafufua kutoka makaburini mwao?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net