Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 28

As-Sajda 32:28

السجدة

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا ٱلْفَتْحُ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ

Maana

Wanasema: Ushindi huu ni lini, kama nyinyi ni wakweli?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanasema: Ushindi huu ni lini, kama mnasema kweli? [28]

[28] Na washirikina wanakwambia wewe na Waumini: Wakati gani Mwenyezi Mungu atakufungulieni mpate ushindi? Twambieni wakati wake ikiwa nyinyi ni wasema kweli.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hawa washirikina wanaifanyia haraka adhabu, wanasema, «Ni lini hukumu hii ya kutuadhibu, kama mnavyodai, ambayo itaamua baina yetu na nyinyi, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net