Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 29

As-Sajda 32:29

السجدة

قُلْ يَوْمَ ٱلْفَتْحِ لَا يَنفَعُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِيمَـٰنُهُمْ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ

Maana

Sema: Siku ya Ushindi, wale waliokufuru imani yao haitawafaa kitu, wala wao hawatapewa muhula.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Siku ya Ushindi, wale walio kufuru imani yao haitawafaa kitu, wala wao hawatapewa muhula. [29]

[29] Waambie: Siku ya hukumu na kufafanua ikikufikilieni, walio kufuru haitowafaa kitu imani yao, wala hawatapewa muhula hata chembe ya hiyo adhabu wanayo istahiki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waambie, ewe Mtume, «Siku ya hukumu ambayo mtateswa na mtashuhudia kifo, makafiri hakutawafaa kuamini kwao, wala hawatacheleweshwa ili watubie na warudie».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net