Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 30

As-Sajda 32:30

السجدة

فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَٱنتَظِرْ إِنَّهُم مُّنتَظِرُونَ

Maana

Basi wapuuze, nawe ngoja; hakika wao wanangoja.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi wapuuze, nawe ngonja; hakika wao wanangoja. [30]

[30] Na ikiwa kufanya maskhara kama hivi ndio mtindo wao, basi wapuuzilie mbali. Na wewe ngojea ukweli aliyo kuahidi Mola wako Mlezi juu yao, kwani wao wanakungojea ushindwe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi wape mgongo, ewe Mtume, hawa washirikina, na usiujali ukanushaji wao, na ungojee vile Allah Mtukufu Atawafanya. Hakika wao ni wenye kungojea na kutaraji mpatwe na jambo baya. Basi Allah Mtukufu Atawapa fedheha na Atawadhalilisha na Akupe ushindi juu yao. Na Allah Mtukufu Ashalifanya hilo, sifa njema ni Zake na wema ni Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net