Al-Ahzaab 33:1
الأحزابيَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ ٱتَّقِ ٱللَّهَ وَلَا تُطِعِ ٱلْكَـٰفِرِينَ وَٱلْمُنَـٰفِقِينَ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا
Ewe Nabii, mche Mwenyezi Mungu wala usiwatii makafiri na wanafiki. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ewe Nabii! Mche Mwenyezi Mungu wala usiwat'ii makafiri na wanaafiki. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima. [1]
[1] Ewe Nabii endelea hivyo hivyo, kama ulivyo, kumcha Mwenyezi Mungu, wala usiyakubali mawazo ya makafiri na wanaafiki. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuvizunguka vitu vyote kwa kuvijua, ni Mwenye hikima katika kauli yake na vitendo vyake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ewe Nabii! Endelea kumcha Allah Mtukufu daima kwa kuyafanya maamrisho Yake na kujiepusha na makatazo Yake, na waumini wakufuate kwa kuwa wao wanahitajia hilo zaidi kuliko wewe, na usiwatii makafiri na watu wa unafiki. Hakika Allah Mtukufu ni Mjuzi wa kila kitu, ni Mwenye hekima katika uumbaji Wake, amri Zake na uendeshaji mambo Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net