Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 13

As-Sajda 32:13

السجدة

وَلَوْ شِئْنَا لَـَٔاتَيْنَا كُلَّ نَفْسٍ هُدَىٰهَا وَلَـٰكِنْ حَقَّ ٱلْقَوْلُ مِنِّى لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ ٱلْجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ أَجْمَعِينَ

Maana

Na lau tungelitaka, tungempa kila mtu uongofu wake. Lakini imekwisha kuwa kauli iliyotoka kwangu: Kwa yakini nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa, majini na watu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau tungeli taka tunge mpa kila mtu uwongofu wake. Lakini imekwisha kuwa kauli iliyo toka kwangu : Kwa yakini nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa, majini na watu. [13]

[13] Na lau kuwa tunataka tungeli mpa kila mtu uwongofu wake, lakini kauli yangu ilikwisha tangulia, nayo ni: Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa majini na watu. Kwa kuwa tulijua kuwa wengi wao watakhiari upotovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau tungetaka tungewapa washirikina hawa uongofu wao na tungewaonyesha njia ya Imani, lakini limethibiti neno linalotoka kwangu na limepasa kwamba nitaujaza, moto wa jahanamu, viumbe wote wa aina mbili, ya kijini na kibanadamu, wenye kukufuru na kuasi, kwa kuwa walichagua upotevu na kuacha uongofu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net