As-Sajda 32:14
السجدةفَذُوقُوا۟ بِمَا نَسِيتُمْ لِقَآءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَآ إِنَّا نَسِينَـٰكُمْ ۖ وَذُوقُوا۟ عَذَابَ ٱلْخُلْدِ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Basi onjeni kwa vile mlivyousahau mkutano wa Siku yenu hii. Na Sisi hakika tunakusahauni. Basi onjeni adhabu ya milele kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi onjeni kwa vile mlivyo usahau mkutano wa Siku yenu hii. Na Sisi hakika tunakusahauni. Basi onjeni adhabu ya milele kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. [14]
[14] Basi ionjeni adhabu kwa vile mlivyo ghafilika na kukutana nami hii leo. Hakika Sisi tunakuacheni katika adhabu kama watu walio sahauliwa. Na onjeni adhabu ya milele isiyo katika, kwa sababu ya ukafiri wenu na uasi wenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wataambiwa washirikina hawa kwa njia ya kulaumiwa, watakapoingia Motoni, «Basi onjeni adhabu kwa sababu ya kughafilika kwenu na Akhera na kujiingiza kwenu kwenye ladha za dunia, sisi tutawaacha kwenye adhabu leo, na onjeni adhabu ya moto wa Jahanamu isiyomalizika kwa yale mliokuwa mkiyafanya duniani ya kumkanusha Allah Mtukufu na kumuasi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net