As-Sajda 32:15
السجدةإِنَّمَا يُؤْمِنُ بِـَٔايَـٰتِنَا ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا۟ بِهَا خَرُّوا۟ سُجَّدًا وَسَبَّحُوا۟ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ۩
Hakika wanaoziamini Aya zetu ni hao tu ambao wakikumbushwa hizo, basi wao huanguka kusujudu, na humsabihi Mola wao Mlezi kwa kumhimidi, nao hawajivuni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wanao ziamini Aya zetu ni hao tu ambao wakikumbushwa hizo, basi wao huanguka kusujudu, na humsabihi Mola wao Mlezi kwa kumhimidi, nao hawajivuni. [15]
[15] Hakika wanazisadiki Ishara zetu wale ambao wanapo waidhiwa kwazo huanguka chini kwa kumsujudia Mwenyezi Mungu, na wakamtakasa Mola wao Mlezi na kila upungufu, na wakamsifu kwa kila ukamilifu. Na wala wao hawatakabari wakakataa kuzifuata Ishara hizi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa kweli, wanaoziamini aya za Qur’ani na kuzifuata kivitendo ni wale ambao wanapowaidhiwa nazo au wanaposomewa, wanamsujudia Mola wao kwa kumnyenyekea na kumtii na wanamtakasa Allah Mtukufu kwa kumsifu katika kusujudu kwao, na hali wao hawaoni kiburi wakaacha kumsujudia na kumtakasa na kumuabudu Yeye Peke Yake Asiyekuwa na mshirika.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net