As-Sajda 32:16
السجدةتَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ ٱلْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَـٰهُمْ يُنفِقُونَ
Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na kutumaini, na hutoa kutokana na tulivyowaruzuku.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na kutumaini, na hutoa kutokana na tulivyo waruzuku. [16]
[16] Mbavu zao zinabambatuka na vitanda vyao, yaani wanaacha usingizi wao, kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa kuikhofu ghadhabu yake, na kutumai rehema yake; na ambao kutokana na mali tuliyo wapa wanatoa kwa ajili ya mambo ya kheri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mbavu za hawa wanaoziamini aya za Allah Mtukufu zinayahama magodoro ya kulalia, wakiswali kwa Mola wao swala ya usiku, wakimuomba kwa kuogopa adhabu na kutarajia malipo mema, na katika kile tulichowaruzuku wanatumia katika kumtii Allah Mtukufu na katika njia Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net