As-Sajda 32:12
السجدةوَلَوْ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلْمُجْرِمُونَ نَاكِسُوا۟ رُءُوسِهِمْ عِندَ رَبِّهِمْ رَبَّنَآ أَبْصَرْنَا وَسَمِعْنَا فَٱرْجِعْنَا نَعْمَلْ صَـٰلِحًا إِنَّا مُوقِنُونَ
Na ungeliwaona wakosefu wanavyoinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao Mlezi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Tumeshaona, na tumeshasikia. Turejeshe tukatende mema, kwani hakika sisi tumekwisha kuwa na yakini sasa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ungeli waona wakosefu wanvyo inamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao Mlezi, (wakisema): Mola wetu Mlezi! Tumesha ona, na tumesha sikia. Turejeshe tukatende mema, kwani hakika sisi tumekwisha kuwa na yakini sasa. [12]
[12] Lau kuwa umejaaliwa kuwaona wakosefu kwenye msimamo wa hisabu ungeli ona ajabu. Pale wale wakosefu wenye kujivuna watavyo inamisha vichwa vyao kwa hizaya inayo tokana na Mola wao Mlezi, nao watasema kwa unyonge: Ewe Mola wetu Mlezi! Tumekwisha yaona tuliyo kuwa na upofu nayo, na tumekwisha yasikia tuliyo kuwa na uziwi nayo, basi turejeshe duniani tupate tenda mema ambayo tuliyo kuwa hatuyatendi. Hakika sasa hivi sisi tumeyakinika na walio kuja nayo Mitume wako.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau ungeona, ewe mhutubiwa, pindi wahalifu waliokanusha kufufuliwa wakiwa wameviinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao kutokana na fedheha na aibu huku wanasema, Mola wetu! Tumeyaona machafu yetu na tumesikia kutoka kwako ukweli wa yale waliokuwa Mitume wako wakituamrisha duniani, na tumeshatubia kwako, basi turudishe duniani ili tufanye matendo ya utiifu kwako. Sisi tushayaamini sasa yale tuliokuwa tukiyakanusha ya kuwa wewe ni mmoja na kwamba wewe utawafufua walio makaburini. Na lau ungeyaona, ewe mhutubiwa, haya yote ungeona jambo kubwa na janga zito.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net