Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 11

As-Sajda 32:11

السجدة

قُلْ يَتَوَفَّىٰكُم مَّلَكُ ٱلْمَوْتِ ٱلَّذِى وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ

Maana

Sema, "Atakufisheni Malaika wa mauti aliyewakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliye wakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi. [11]

[11] Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti, aliyewakilishwa kuzikamata roho zenu utapo kwisha muda wenu. Kisha kwa Mwenyezi Mungu peke yake ndio mtarejea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, Atakayewafisha nyinyi ni Malaika wa kifo aliyewakilishwa kwenu, atakayezichukua roho zenu utakapokoma muda wenu wa kuishi, na hamtachelewa hata kidogo, kisha mtarudishwa kwa Mola wenu, Awalipe kwa matendo yenu, yakiwa ni mema Awalipe wema na yakiwa maovu Awalipe uovu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net