Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 10

As-Sajda 32:10

السجدة

وَقَالُوٓا۟ أَءِذَا ضَلَلْنَا فِى ٱلْأَرْضِ أَءِنَّا لَفِى خَلْقٍ جَدِيدٍۭ ۚ بَلْ هُم بِلِقَآءِ رَبِّهِمْ كَـٰفِرُونَ

Maana

Nao walisema: "Kwani tutakapokwishapotelea chini ya ardhi, ni kweli kwamba tutarudishwa katika umbo jipya?" Bali wao wanakufuru kukutana na Mola wao Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nao husema: Tutapo kwisha potea chini ya ardhi, ni kweli tutarudishwa katika umbo jipya? Bali wao wanakanusha kwamba watakutana na Mola wao Mlezi. [10]

[10] Na wanao kanya kufufuliwa wakasema: Ati sisi tukisha kuwa mchanga, ulio changanyika na mchanga wa ardhi, usibagulike, ndio kweli tutarejea kwa umbo jipya? Hao hakika si kama wanakanya kufufuliwa tu, bali wanakadhibisha yote yatayo kuwako Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wenye kumshirikisha Allah Mtukufu wenye kukanusha kufufuliwa wamesema, «Je, itakapokuwa mchanga nyama yetu na mifupa yetu, je, tutafufuliwa tuwe umbo lingine?» huku wakiona kuwa hilo liko mbali kutokea na huku hawataki kuifikia haki. Na hilo kwao ni udhalimu na ushindani, hii ni kwamba wao wanakanusha kukutana na Mola wao Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net