Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 9

As-Sajda 32:9

السجدة

ثُمَّ سَوَّىٰهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِن رُّوحِهِۦ ۖ وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمْعَ وَٱلْأَبْصَـٰرَ وَٱلْأَفْـِٔدَةَ ۚ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ

Maana

Kisha akamtengeneza sawasawa, na akampulizia katika roho yake, na akawajalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyoshukuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru. [9]

[9] Kisha akamsimamisha na kumkuza, na akamtia ndani yake siri yake aliyo mkhusisha nayo, na akakupeni masikio, na macho, na akili, mpate kusikia na kuona na kufahamu. Nanyi hamshukuru ila kwa uchache.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha Aliukamilisha uumbaji wa binadamu na Akaufanya upendeze na Akalifanya zuri umbo lake, na Akapuliza ndani yake roho Yake kwa kumtuma Malaika kwake ili apulize roho, na Akawapa nyinyi, enyi watu, neema ya masikizi na maangalizi ya kupambanua sauti, rangi, vitu na watu, na neema ya akili ya kupambanua jema na baya na lenye kunufaisha na kudhuru. Ni kuchache kule kumshukuru kwenu Mola wenu kwa neema Alizowapatia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net