Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 8

As-Sajda 32:8

السجدة

ثُمَّ جَعَلَ نَسْلَهُۥ مِن سُلَـٰلَةٍ مِّن مَّآءٍ مَّهِينٍ

Maana

Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji dhaifu yanayodharauliwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji madhaifu. [8]

[8] Kisha akawafanya dhuriya zake wa namna mbali mbali kutokana na maji machache, dhaifu, yasiyo tamanika kwa kawaida. Katika Aya hii tukufu "utokane na kizazi cha maji dhaifu". Neno la Kiarabu lilio tumiwa ni "Mahiin". Neno hili likitumiwa kwa mtu lina maana ya "dhaif", mnyonge, na pia lina maana ya "chache". Basi kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Min maain mahiin" maana yake ni "kutokana na maji machache dhaifu" , ndiyo ya kudharauliwa. Mfano wa hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Au mimi si bora kuliko huyu aliye (mahiin) mnyonge wala hawezi kusema waziwazi?" (Azzukhruf: 43.52). Na neno "Mahana al-ibila" maana yake "Kamkama maziwa ngamia". Kwa hivyo basi hapana ubaya kulifasiri neno hili Mahiin katika Aya hii kwa maana ya maji yanayo toka kwa kuchupa, au kumiminika, (kama yanavyo toka maziwa kwenye chuchu) au machache.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha Akavifanya vizazi vya Ãdam vizalikane na tone dhaifu lililo dogo na dhalili.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net