Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 93

Aal-i-Imraan 3:93

آل عمران

كُلُّ ٱلطَّعَامِ كَانَ حِلًّا لِّبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ إِلَّا مَا حَرَّمَ إِسْرَٰٓءِيلُ عَلَىٰ نَفْسِهِۦ مِن قَبْلِ أَن تُنَزَّلَ ٱلتَّوْرَىٰةُ ۗ قُلْ فَأْتُوا۟ بِٱلتَّوْرَىٰةِ فَٱتْلُوهَآ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ

Maana

Kila chakula kilikuwa halali kwa Wana wa Israili isipokuwa kile alichojiharamishia Israili mwenyewe kabla ya kuteremshwa Taurati. Sema: Ileteni Taurati, na muisome ikiwa nyinyi ni wakweli.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kila chakula kilikuwa halali kwa Wana wa Israili isipo kuwa alicho jizuilia Israili mwenyewe kabla haijateremshwa Taurati. Sema: Leteni Taurati muisome ikiwa nyinyi ni wasema kweli. [93]

[93] Mayahudi waliwatoa kombo Waislamu kwa kuhalalisha baadhi ya vyakula kama nyama ya ngamia na maziwa yake. Wakadai kuwa hayo yaliharimishwa na sharia ya Ibrahim. Mwenyezi Mungu Subhanahu aliwarudi madai yao hayo kwa kubainisha kuwa vyakula vyote vilikuwa halali kwa Wana wa Yaakub (ndiye Israil) kabla ya kuteremka Taurati, ila alicho jizuia Yaakub mwenyewe kwa sababu zilizo mkhusu yeye tu, basi na wao wakijiharimishia nafsi zao. Mwenyezi Mungu akamuamrisha Nabii wake awatake walete uthibitisho wa Taurati kuwa sharia ya Ibrahim imeharimisha hayo kama wao wanasema kweli. Wakashindwa, wakanywea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Vyakula vyote vizuri vilikuwa ni halali kwa wana wa Ya‛qûb, amani imshukiye, isipokuwa vile ambavyo Ya‛qûb alijiharamishia yeye mwenyewe kwa sababu ya ugonjwa uliompata. Na hayo yalikuwa kabla ya Taurati haijateremshwa. Taurati ilipoteremshwa, Allah Mtukufu Aliwaharamishia Wana wa Isrãîl baadhi ya vyakula vilivyokuwa halali kwao. Na hilo ni kwa sababu ya dhuluma zao na uovu wao. Waambie, ewe Mtume, Ileteni Taurati na muyasome yaliyomo ndani yake iwapo muna hakika ya madai yenu kwamba Allah Mtukufu ameteremsha humo uharamu wa aliojiharamishia Ya‛qûb nafsi yake, ili mpate kuujua ukweli wa yale yaliyokuja katika Qur’ani ya kwamba Allah Mtukufu Hakuwaharamishia Wana wa Isrãîl chochote kabla ya kuteremka Taurati, isipokuwa yale ambayo Ya‛qûb alijiharamishia nafsi yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net