Aal-i-Imraan 3:94
آل عمرانفَمَنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ
Na mwenye kumzulia uongo Mwenyezi Mungu baada ya hayo, basi hao ndio madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu baada ya hayo, basi hao ndio madhaalimu. [94]
[94] Ilipo thibiti kuwa wameemewa basi wenye kumsingizia uwongo Mwenyezi Mungu baada ya hoja hizo, hao ndio walio selelea na udhaalimu wao, na wanastahiki kuitwa Madhaalimu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi yule atakayemzulia Allah Mtukufu urongo baada ya kuisoma Taurati na ukweli kuwa wazi, basi hao ndio madhalimu wanaomzulia Allah Mtukufu ya batili.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net