Aal-i-Imraan 3:95
آل عمرانقُلْ صَدَقَ ٱللَّهُ ۗ فَٱتَّبِعُوا۟ مِلَّةَ إِبْرَٰهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ
Sema: Mwenyezi Mungu amesema kweli. Basi fuateni mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mwenyezi Mungu amesema kweli. Basi fuateni mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. [95]
[95] Baada ya kushindwa kwao Mwenyezi Mungu amemuamrisha Nabii wake awabainishie kuwa ukweli wa Mwenyezi Mungu umethibiti katika ayasemayo. Basi ifuateni Sharia ya Ibrahim anayo kutakeni muifuate, na nyinyi mnaikanusha. Hii ni mbali kabisa na hizo Dini za uwongo, kwani Ibrahim hakuwa miongoni mwa washirikina.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waambie, ewe Mtume, Allah Mtukufu Amesema kweli katika Aliyoyatolea habari na yale ya Sheria Aliyoipitisha. Basi iwapo nyinyi ni wakweli katika mahaba yenu na kujinasibisha kwenu na rafiki halisi wa Allah Mtukufu, Ibrãhîm, amani imshukiye, fuateni mila yake Aliyoipitisha Allah Mtukufu kupitia kwa ulimi wa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie. Kwani hiyo ndiyo haki isiyokuwa na shaka. Na wala hakuwa Ibrãhîm, amani imshukie, ni kati ya wale wanaomshirikisha Allah Mtukufu, katika kumpwekesha na kumuabudu, na yoyote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net