Aal-i-Imraan 3:96
آل عمرانإِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِى بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَـٰلَمِينَ
Hakika, Nyumba ya kwanza waliyowekewa watu kwa ibada ni ile iliyo Bakka, iliyobarikiwa na yenye uongofu kwa walimwengu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, (Makka) iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote. [96]
[96] Katika kufuata mila ya Ibrahim ni kuelekea wakati wa Swala Nyumba aliyo ijenga, na kwenda kuhiji huko. Mwenyezi Mungu amebainisha hayo kwa kusema: Hakika Nyumba ya awali kwa ukongwe na utukufu aliyo ijaalia Mwenyezi Mungu iwe ni ya ibada kwa watu ni hiyo iliyoko Makka (au Bakka kama pia inavyoitwa). Nayo ina kheri nyingi na manufaa, na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ameijaalia iwe na baraka. Nayo Nyumba hiyo ni pahali pa uwongofu kwa watu kwa kuhiji na kuelekea wakati wa Swala.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika nyumba ya mwanzo iliyojengwa kwa ajili ya kumuabudu Allah Mtukufu ni hiyo nyumba ya Allah Mtukufu takatifu iliyoko Maka. Na nyumba hiyo imebarikiwa, mema huko huongezwa na rehema huko hushuka. Na katika kuielekea nyumba hiyo kwenye Swala na kuiendea kipindi cha kutekeleza Hija na Umra, pana wema na uongofu kwa watu wote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net