Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 97

Aal-i-Imraan 3:97

آل عمران

فِيهِ ءَايَـٰتٌۢ بَيِّنَـٰتٌ مَّقَامُ إِبْرَٰهِيمَ ۖ وَمَن دَخَلَهُۥ كَانَ ءَامِنًا ۗ وَلِلَّهِ عَلَى ٱلنَّاسِ حِجُّ ٱلْبَيْتِ مَنِ ٱسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ عَنِ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Ndani yake kuna Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim. Na mwenye kuingia humo, anakuwa na amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewawajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezaye njia ya kuiendea. Na atakayekufuru, basi hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu. [97]

[97] Zipo dalili wazi za kuonyesha utakatifu wake huo Msikiti wa Makka na kuzidi fadhila zake. Miongoni mwa hizo ni hapo alipo kuwa akisimama Nabii Ibrahim a.s. kwa kuswali. Na pia kuwa anaye ingia humo huwa amesalimika halimpati ovu. Na kuhiji Makka ni waajibu wa kila mtu awezae kwenda. Na mwenye kukataa, akaiasi amri ya Mwenyezi Mungu, na akaipinga Dini yake, basi khasara itamuangukia mwenyewe, na Mwenyezi Mungu anajitosha, hawahitajii watu wote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Katika Nyumba hii kuna alama waziwazi ya kwamba hiyo ni katika ujenzi wa Ibrãhîm na kwamba Allah Mtukufu ameitukuza na kuipa heshima. Kati ya alama hizo ni Maqãm ya Ibrãhîm, amani imshukie, nayo ni lile jiwe ambalo alikuwa akisimama juu yake wakati alipokuwa akiziinua nguzo za Alkaba, yeye na mwanawe Ismã‘îl. Na yoyote mwenye kuingia Nyumba hii atapata amani ya nafsi yake, hapana yoyote atakayemkusudia kwa uovu. Na Allah Mtukufu Amewajibisha kwa mwenye uwezo katika watu, popote atakapokuwa kuiendea nyumba hii ili kutekeleza matendo ya Hija. Na yoyote mwenye kuikanusha faradhi ya Hija, basi huyo amekufuru. Na Allah Mtukufu ni Mkwasi, Hana haja ya hija yake wala amali yake na wala Hana haja na viumbe vyake vyote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net