Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 98

Aal-i-Imraan 3:98

آل عمران

قُلْ يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعْمَلُونَ

Maana

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnazikufuru ishara za Mwenyezi Mungu, na ilhali Mwenyezi Mungu ni Shahidi kwa yote mnayoyatenda?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnakanusha ishara za Mwenyezi Mungu, na ilhali kuwa Mwenyezi Mungu ni Shahidi kwa yote mnayo yatenda? [98]

[98] Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la amemuamrisha Mtume wake awahizi Watu wa Kitabu kwa kuendelea kwao kukufuru na kupotoka na kupotosha, akasema: Enyi Watu wa Kitabu! Huo ukafiri wenu hauna sura wala maana. Kwa sababu gani mnakanusha dalili, na hoja za Mwenyezi Mungu zenye kuthibitisha Unabii na Ukweli wa Muhammad? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuvijua vitendo vyenu na atakulipeni malipo yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliopewa vitabu kati ya Mayahudi na Wanaswara, «Kwa nini mnazikanusha hoja za Allah Mtukufu zinazojulisha kwamba dini ya Allah Mtukufu ni Uislamu na mnayakanusha yaliyomo kwenye vitabu vyenu miongoni mwa dalili na hoja juu ya hilo hali ya kuwa nyinyi mnajua? Na Allah Mtukufu ni shahidi juu ya kitendo chenu mnachokifanya.» Katika haya, pana makemeo na ahadi ya adhabu kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net