Aal-i-Imraan 3:99
آل عمرانقُلْ يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ لِمَ تَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ مَنْ ءَامَنَ تَبْغُونَهَا عِوَجًا وَأَنتُمْ شُهَدَآءُ ۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnamzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu aliyeamini mkiitakia ipotoke, ilhali nyinyi mnashuhudia? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika mbali na mnayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnamzuilia aliye amini Njia ya Mwenyezi Mungu mkiitafutia kosa, na hali nyinyi mnashuhudia? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yatenda. [99]
[99] Enyi Watu wa Kitabu! Vipi mnajaribu kumgeuza mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kuifuata Haki aache Njia Iliyo Nyooka ya Mwenyezi Mungu wa Kweli, na mnajaribu kuikosoa Njia hiyo, na nyinyi mnajua kuwa hiyo ndiyo Haki? Wala Mwenyezi Mungu hakughafilika na vitendo vyenu, naye atakulipeni kwavyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia Mayahudi na Wanaswara, «Mbona mnamzuia kuingia katika Uislamu yule mtu atakaye hivyo na mnamtakia upotofu na kupinduka kwenye lengo na muelekeo wa kisawa, na nyinyi mnajua kwamba niliyokuja nayo ndiyo haki?» Basi, Allah Mtukufu si mwenye kughafilika kwa mnayoyatenda, na Atawalipa kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net