Aal-i-Imraan 3:100
آل عمرانيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تُطِيعُوا۟ فَرِيقًا مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ يَرُدُّوكُم بَعْدَ إِيمَـٰنِكُمْ كَـٰفِرِينَ
Enyi mlioamini! Mkilitii kundi katika wale waliopewa Kitabu, watawarudisha baada ya kuamini kwenu muwe makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Mkiwat'ii baadhi ya walio pewa Kitabu watakurudisheni kuwa makafiri baada ya Imani yenu. [100]
[100] Mwenyezi Mungu anawahadharisha Waumini na vitimbi vya baadhi ya Watu wa Kitabu,(Mayahudi na Wakristo), vya uchochezi wao wa udanganyifu kwa kusema: Mkiwat'ii baadhi ya Watu wa Kitabu katika yale wanayo yaeneza ya kutilisha shaka katika Dini yenu, itakuwa mnarajea tena kwenye upotovu baada ya uwongofu, na wakurejezeni muwe makafiri baada ya kuwa ni Waumini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazitumia Sheria Zake kwa kuzifuata, iwapo mtalitii kundi la Mayahudi na Wanaswara, miongoni mwa wale ambao Allah Mtukufu Amewapa Taurati na Injili, watawapoteza na watawatia shaka katika dini yenu, ili mupate kurudi nyuma na kuikanusha haki baada ya kuwa mlikuwa waumini wa haki hiyo, basi msiwaamini juu ya dini yenu wala msiwakubalie rai yoyote au shauri.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net