Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 101

Aal-i-Imraan 3:101

آل عمران

وَكَيْفَ تَكْفُرُونَ وَأَنتُمْ تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ ءَايَـٰتُ ٱللَّهِ وَفِيكُمْ رَسُولُهُۥ ۗ وَمَن يَعْتَصِم بِٱللَّهِ فَقَدْ هُدِىَ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

Maana

Na vipi mkufuru hali ya kuwa nyinyi mnasomewa Aya za Mwenyezi Mungu, na Mtume wake yuko miongoni mwenu? Na mwenye kushikamana na Mwenyezi Mungu, basi huyo hakika ameongolewa kwenye Njia iliyonyooka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na vipi mkufuru hali nyinyi mnasomewa Aya za Mwenyezi Mungu na Mtume yuko kati yenu? Na mwenye kushikamana na Mwenyezi Mungu basi huyo ameongozwa kwenye Njia Iliyo Nyooka. [101]

[101] Hebu izingitieni hali yenu ya ajabu, kuwa mnapotoka na mnakufuru baada ya Imani, na hali mnasomewa Qur'ani, na Mtume mnaye, anakubainishieni na anakukingeni na upotovu katika Dini yenu. Na mwenye kumkimbilia Mola wake Mlezi, na akashikamana na Dini yake, basi huyo amefanya vyema. Mola wake Mlezi amemwongoa kwenye Njia ya kufuzu na kufaulu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na vipi mtamkufuru Allah Mtukufu, enyi Waumini, ilhali mnasomewa aya za Qur’ani, na Mtume wa Allah Mtukufu, Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, anazifikisha aya hizo kwenu? Na yoyote atakayetegemea kwa Allah Mtukufu, akashikamana na Qur’ani na mafundisho ya Mtume (Sunnah), basi huyo ameafikiwa kufuata njia iliyo wazi na mpango uliolingana sawa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net