Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 102

Aal-i-Imraan 3:102

آل عمران

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِۦ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ

Maana

Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu haki ya kumcha, wala kamwe msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife ila nanyi ni Waislamu. [102]

[102] Hakika mlango wa shari uwazi ikiwa hamumchi Mwenyezi Mungu. Basi enyi mlio amini! Mkhofuni Mwenyezi Mungu kwa khofu inayopasa, kwa kutenda anayo amrisha, na kuyaepuka anayo yakataza. Na dumuni juu ya Uislamu mpaka mtakapo kutana na Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi ambao mumemuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake, muogopeni Allah Mtukufu kwa namna inavyopasa mumuogope. Nako ni Atiiwe wala Asiasiwe, Ashukuriwe wala asikufuriwe na Akumbukwe wala Asisahauliwe. Na dumuni katika kushikamana na Uislamu wenu mpaka mwisho wa uhai wenu, ili mkutane na Allah Mtukufu na nyinyi muko katika hali hiyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net