Aal-i-Imraan 3:103
آل عمرانوَٱعْتَصِمُوا۟ بِحَبْلِ ٱللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا۟ ۚ وَٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَآءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِۦٓ إِخْوَٰنًا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ ٱلنَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ
Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msitengane. Na ikumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu: Mlipokuwa maadui nyinyi kwa nyinyi, naye akaziunganisha nyoyo zenu; na kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa kwenye ukingo wa shimo la Moto, naye akawaokoa kutokana nao. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowabainishia Ishara zake ili mpate kuongoka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka. [103]
[103] Nyote nyinyi shikamaneni na Dini ya Mwenyezi Mungu, wala msifanye jambo litalo leta mfarakano baina yenu. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu mlivyo kuwa wakati wa ujahili nyinyi kwa nyinyi maadui. Mwenyezi Mungu akaziunganisha nyoyo zenu kwa Uislamu, mkawa mnapendana, na ilhali kwa sababu ya ukafiri wenu na kufarikiana kwenu mlikuwa juu ya ukingo wa Moto, akakuokoeni kwa Uislamu. Kwa mfano wa bayana kama hii ya pekee Mwenyezi Mungu anakubainishieni daima njia za kheri, ili mdumu katika uwongofu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Shikamaneni nyote na Kitabu cha Mola wenu na uongofu wa Mtume wenu, wala msitende ambayo yatapelekea kutengana kwenu. Na ikumbukeni neema kubwa ambayo Allah Mtukufu Amewaneemesha nayo, pindi mlipokuwa, enyi Waumini, kabla ya Uislamu ni maadui, Allah Mtukufu Akazikusanya nyoyo zenu juu ya kumpenda Yeye na kumpenda Mtume Wake, na akatia ndani ya nyoyo zenu mahaba ya kupendana wenyewe kwa wenyewe, hapo mkawa, kwa fadhila Zake, ni ndugu mpedanao. Na mlikuwa kwenye ukingo wa moto wa Jahanamu, Allah Mtukufu Akawaongoza kwa Uislamu na Akawaokoa na Moto. Na kama Allah Mtukufu Alivyowafunulia wazi alama za imani iliyo sahihi, hivyo hivyo Anawabainishia yote yale ambayo ndani yake muna kutengenea kwenu, mpate kuongoka kweye njia ya uongofu na mpate kuiandama ili msipotee.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net